Italia - Wikipedia, kamusi elezo huru
Nenda kwa yaliyomo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Italia
Repubblica Italiana (
Kiitalia
Bendera
Nembo
Wimbo wa taifa:
"Il Canto degli Italiani" (
Kiitalia
"Wimbo wa Waitalia"
Eneo la Italia katika bara la Ulaya
Mji mkuu
na mkubwa
Roma
Lugha rasmi
Kiitalia
Kabila
91.0% Raia wa Italia
9.0% Wengine
Dini
84%
Ukristo
12%
Wasio na dini
1%
Uislamu
3% Nyinginezo
Uraia
Mwitalia
Serikali
Jamhuri ya Muungano wa Rais
Sergio Mattarella
Rais
Ignazio La Russa
Rais
wa
Seneti
Historia
Muungano
17 Machi 1861
Jamhuri
12 Juni 1946
Katiba ya sasa
1 Januari 1948
Eneo
Jumla
km
301,340
Msongamano
195/km
PLT
PPP
Kadirio la 2024
Jumla
$3.597 Trilioni
Kwa kila mtu
$60,992
PLT
Kawaida
Kadirio la 2024
Jumla
$2.376 Trilioni (ya 8)
Kwa kila mtu
$40,286
HDI
(2022
0.906
juu sana
Gini
(2021)
34.8
Sarafu
Euro
EU
Majira ya saa
UTC
+1 (CET)
Msimbo wa simu
+39
Jina la kikoa
.it
Italia
jina rasmi
Jamhuri ya Italia
) ni
nchi
iliyopo
kusini
mwa
Ulaya
. Inapakana na
Ufaransa
upande wa
magharibi
Uswisi
na
Austria
upande wa
kaskazini
, na
Slovenia
upande wa
mashariki
. Nchi hii ina
idadi
ya watu takriban milioni 60 na ina eneo la
kilomita za mraba
301,340.
Roma
jiji
kubwa zaidi, pia ni
mji mkuu
. Italia imegawanywa katika
mikoa 20
na inajulikana kwa
alama
zake za
kihistoria
sanaa
vyakula
, na kama mahali pa kuzaliwa kwa
Dola la Roma
na
Renaissance
Italia ina
urithi
tajiri wa
kitamaduni
unaoendelea kuathiri
dunia
hadi leo. Kuanzia
usanifu majengo
na
uhandisi
wa
Roma ya Kale
hadi kazi bora za enzi ya
Renaissance
kutoka kwa wasanii kama
Leonardo da Vinci
na
Michelangelo
, mchango wa Italia katika sanaa,
fasihi
na
sayansi
hauna kifani.
Miji
kama
Firenze
Venezia
na
Milano
inajulikana kwa
majumba
ya kihistoria,
makanisa
, na maeneo ya kale yenye hazina ya sanaa, na huvutia
mamilioni
ya
watalii
kila mwaka.
Uchumi
wa Italia ni miongoni mwa mikubwa zaidi katika
Umoja wa Ulaya
na unajulikana kwa sekta mbalimbali kama vile
mitindo
ya
mavazi
magari
kilimo
na utalii. Italia ni makao ya chapa maarufu duniani kama
Ferrari
Gucci
na Lavazza. Nchi hii pia ina nafasi muhimu katika
siasa
za kimataifa kama mwanachama
mwanzilishi
wa
Umoja wa Ulaya
NATO
na
Umoja wa Mataifa
. Licha ya changamoto za kiuchumi, Italia bado ni nchi yenye
uhai
mkubwa, utambulisho imara wa kitaifa na ushawishi mpana wa kitamaduni
duniani
Jiografia
Umbo
la jamhuri, kama lile la
rasi
yake, linafanana na
mguu
linalozungukwa na
maji
ya
Mediteraneo
pande
tatu
Milima
ya
Appennini
inaunda
uti wa mgongo
wake, wakati ile ya
Alpi
, ambayo ni mirefu zaidi, inaunda kwa kiasi kikubwa mpaka kati ya Italia na nchi nyingine za
Ulaya
Mlima mrefu zaidi, ukiwa na
mita
4,810 juu ya
usawa wa bahari
, unaitwa
Monte Bianco
(Mlima Mweupe) na uko mpakani kwa Ufaransa.
Visiwa
viwili vikubwa vya
Sisilia
na
Sardinia
ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vingi vidogovidogo, vile vya
Pelagie
na
Pantelleria
vikiwa upande wa
Afrika
Italia ina
volkeno
14, ambazo 4 kati yake ziko hai: ile ndefu zaidi kuliko zote za Ulaya (mita 3,329) inaitwa
Etna
na iko
mashariki
mwa Sisilia. Italia inaongoza Ulaya kwa wingi wa
matetemeko ya ardhi
Mto
mrefu zaidi unaitwa
Po
na una
urefu
wa
kilomita
652. Mito mingine mirefu ni
Adige
Tevere
Adda
Oglio
Tanaro
Ticino
Arno
Piave
Reno
Sarca-Mincio
n.k.
Maziwa
makubwa zaidi ni:
Garda
(km
367.94),
Ziwa Maggiore
(212.51, likiingia Uswisi),
Ziwa la Como
(145.9),
Trasimeno
(124.29) na
Ziwa la Bolsena
(113.55).
Kutokana na
urefu
mkubwa wa Italia toka
kaskazini
hadi
kusini
hali ya hewa
ni tofauti sana, kuanzia
baridi
kali sana hadi
joto
kali sana.
Mikoa
Bendera
Jina
Makao makuu
Eneo (km
Wakazi
Msongamano wa watu/km²
Wilaya
Miji
Miji mikubwa
Hali ya utawala
Abruzzo
L'Aquila
10,763
1,307,919
122
305
Kawaida
Bonde la Aosta
Aosta
3,263
126,933
39
74
Kujitawala
Puglia
Bari
19,358
4,045,949
209
258
Bari
Kawaida
Basilicata
Potenza
9,995
575,902
58
131
Kawaida
Calabria
Catanzaro
15,081
1,954,403
130
409
Reggio Calabria
Kawaida
Campania
Napoli
13,590
5,761,155
424
551
Napoli
Kawaida
Emilia-Romagna
Bologna
22,446
4,354,450
194
348
Bologna
Kawaida
Friuli-Venezia Giulia
Trieste
7,858
1,219,356
155
218
Trieste
Kujitawala
Lazio
Rome
17,236
5,550,459
322
378
Rome
Kawaida
Liguria
Genoa
5,422
1,565,349
289
235
Genoa
Kawaida
Lombardia
Milan
23,861
9,749,593
409
12
1544
Milan
Kawaida
Marche
Ancona
9,366
1,541,692
165
239
Kawaida
Molise
Campobasso
4,438
312,394
70
136
Kawaida
Piemonte
Turin
25,402
4,366,251
172
1206
Turin
Kawaida
Sardinia
Cagliari
24,090
1,637,193
68
377
Cagliari
Kujitawala
Sisilia
Palermo
25,711
4,994,817
194
390
Catania
Messina
Palermo
Kujitawala
Trentino-Alto Adige/Südtirol
Trento
13,607
1,036,707
76
333
Kujitawala
Toscana
Firenze
22,994
3,679,027
160
10
287
Firenze
Kawaida
Umbria
Perugia
8,456
885,535
105
92
Kawaida
Veneto
Venisi
18,399
4,865,380
264
581
Venisi
Kawaida
Historia
Makala kuu:
Historia ya Italia
Mji wa
Venisi
, uliojengwa juu ya
visiwa
117.
Mnara wa Pisa
, pamoja na
kanisa kuu la Pisa
na
batizio
yake.
Ikulu ya Caserta
Akiolojia
imethibitisha uwepo wa
Homo erectus
miaka 700,000 hivi iliyopita,
Homo neanderthalensis
miaka 200,000 hivi iliyopita.
Homo sapiens sapiens
alifika miaka 40,000 hivi iliyopita.
Kufikia
milenia ya 1 KK
wakazi wengi walikuwa wa
jamii ya Kizungu
na kutumia
lugha za Kihindi-Kiulaya
, ingawa walibaki pia wazao wa wakazi wa awali.
Peninsula
ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na
Jamhuri ya Roma
509
27 KK
), lakini hiyo ilipoenea
Ulaya kusini
na
magharibi
Afrika ya Kaskazini
na
Asia ya Magharibi
ikawa na sura ya kimataifa kama
Dola la Roma
Umoja
ulipotea kuanzia
uvamizi
wa
jiji
la
Roma
uliofanywa na
Wagermanik
476
BK
) na hasa baada ya
ufalme
wa
Karolo Mkuu
aliyetawala sehemu ya
kaskazini
tu.
Juhudi za kuurudisha umoja zilifanywa hasa katika
karne ya 19
, ambapo
Ufalme wa Sardinia
uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka
1860
1866
na
1870
) na kubadilika kuwa
Ufalme wa Italia
wenye
makao makuu
Roma.
Baada ya
vita vikuu vya pili
iligeuka
Jamhuri
yenye
katiba
inayotia
mamlaka
kuu
mikononi
mwa
bunge
Ni kati ya nchi
sita
zilizoanzisha
Umoja wa Ulaya
mwaka
1957
ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa
pesa
ya pamoja (
Euro
).
Sanaa na utalii
Kuanzia kushoto kwa kufuata mzunguko wa mishale katika saa:
Kanisa kuu
la
Florence
, lenye
kuba
la
matofali
kubwa kuliko yote
duniani
Basilika la Mt. Petro
kanisa
kubwa kuliko yote duniani, liko
Vatikani
, nchi inayozungukwa na Italia pande zote;
kanisa kuu la
Milano
, la tano duniani kwa ukubwa;
na Basilika la
Mt. Marko
Venezia
Italia ndiyo nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (61) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya
UNESCO
ya "
Urithi wa Dunia
".
Kwa sababu hiyo pia inashika nafasi ya 5 kati ya nchi zote zilizo lengo la
utalii
Demografia
Mtawanyiko wa watu wenye asili ya Italia.
Wananchi wana sifa za pekee kati ya
Wazungu
wote, hata upande wa
DNA
, kutokana na jiografia na historia ya
rasi
Ni kati ya nchi ambamo watu wanatarajiwa kuishi miaka mingi zaidi, lakini pia ni kati ya nchi ambapo
uzazi
ni mdogo zaidi: wanaokufa ni wengi kuliko wanaozaliwa.
Kutokana na
umati
wa Waitalia waliohama nchi hiyo karne za nyuma, sasa zaidi ya watu
milioni
60 nje ya Italia wana asili ya nchi hiyo, mbali na
raia
zaidi ya milioni 4 wanaoishi nje.
Lugha rasmi
ni
Kiitalia
, inayotegemea zaidi
lahaja
za
Italia ya Kati
, lakini siku hizi inatumiwa na wananchi walio wengi hata katika mikoa mingine, ambayo kwa jumla ni 20. Wananchi wanatumia pia lugha nyingine, kama
Kisardinia
(2.5%),
Kifriuli
(1.2%) na
Kijerumani
(0.6%), na vilevile wahamiaji wanatumia lugha zao asili, hasa
Kiromania
(1.3%),
Kiarabu
(0.8%),
Kialbania
(0.6%) na
Kihispania
(0.4%).
Upande wa
dini
, wengi wao (81.2%) ni
Wakristo
wa
Kanisa Katoliki
, wakifuatwa na
Waorthodoksi
(2.8%, wengi wao wakiwa
wahamiaji
, hasa kutoka
Romania
) na
Waprotestanti
(1.1%, wengi wao wakiwa
Wapentekoste
).
Uhamiaji
mwingi wa miaka ya mwisho wa
karne ya 20
umeleta pia
Uislamu
(3.7%) na
dini
nyingine.
Dini zote zinaachiwa
uhuru
na, tofauti na nchi nyingi za Ulaya, waumini wake wanajitahidi kiasi kufuata
ibada
(29% kila
wiki
).
Serikali
Muundo wa Italia ni
jamhuri
ya
kidemokrasia
ya uwakilishi wa
bunge
, iliyoanzishwa chini ya
Katiba
ya mwaka
1948
Rais
wa Jamhuri ni mkuu wa
nchi
na huchukua nafasi ya mdhamini wa Katiba, huku
Waziri Mkuu
(Rais wa Baraza la Mawaziri) akiwa mkuu wa
serikali
. Waziri Mkuu huteuliwa na Rais na ni lazima apate
imani
ya
matawi
mawili ya Bunge la Italia ili aweze kuongoza. Mfumo wa
kisiasa
wa Italia umejengwa juu ya mgawanyo wa
madaraka
kati ya mihimili ya utendaji, ya kutunga
sheria
, na ya
mahakama
Tawi la kutunga sheria linaundwa na Bunge lenye mabaraza mawili, ambalo ni Bunge la Wawakilishi na Seneti ya Jamhuri. Mabaraza hayo mawili yana
mamlaka
sawa na yanawajibika kupitisha sheria, kuidhinisha
bajeti
, na kusimamia serikali. Wabunge huchaguliwa na wananchi kupitia mfumo mchanganyiko wa
uchaguzi
. Italia ina
mfumo wa vyama vingi
, jambo linalopelekea kila mara kuundwa kwa serikali za mseto kutokana na uwakilishi wa uwiano unaoruhusu vyama vidogo kupata viti.
Tawi la utendaji linajumuisha Waziri Mkuu na
Baraza la Mawaziri
, ambao wanawajibika kwa sera za
kitaifa
, usimamizi wa shughuli za serikali, na utekelezaji wa sheria.
Wizara
hushughulikia nyanja kama masuala ya nje,
uchumi
ulinzi
, na
elimu
Mamlaka ya mahakama ni huru na haitegemei mihimili mingine ya
dola
, na inajumuisha mahakama za kiraia, za kijinai, na za kiutawala. Mahakama ya Katiba huhakikisha kuwa sheria zinazingatia Katiba ya Italia. Italia pia ni mwanachama wa
Umoja wa Ulaya
, na sheria za umoja huo huathiri sera za ndani, hasa katika masuala ya uchumi na
biashara
Watu maarufu
Fransisko wa Asizi
Marko Polo
Dante Alighieri
Katerina wa Siena
Bernardino wa Siena
Kristofa Columbus
Amerigo Vespucci
Yohane wa Verrazzano
Nikola Machiavelli
Leonardo wa Vinci
Michelangelo
Raffaello Sanzio
Karolo Borromeo
Papa Pius V
Galileo Galilei
Amedeo Avogadro
Alessandro Volta
Giuseppe Verdi
Giuseppe Garibaldi
Yohane Bosco
Antonio Meucci
Papa Pius X
Maria Montessori
Guglielmo Marconi
Benito Mussolini
Enrico Fermi
Papa Yohane XXIII
Papa Paulo VI
Pio wa Pietrelcina
Carlo Rubbia
Tazama pia
Mikoa ya Italia
Orodha ya miji ya Italia
Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
Tanbihi
"Italy GDP profile"
. Iliwekwa mnamo
2025-01-30
"Italy Hdi"
. Iliwekwa mnamo
2025-01-31
"The Duomo of Florence
Tripleman"
. tripleman.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2009-12-06
. Iliwekwa mnamo
25 Machi
2010
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
"Brunelleschi's Dome"
. Brunelleschi's Dome.com
. Iliwekwa mnamo
25 Machi
2010
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
"St. Peter's Basilica (Basilica di San Pietro) in Rome, Italy"
reidsitaly.com
See
List of largest church buildings in the world
; note that the #3 entry,
First Family Church
building in Kansas, is now a school education complex.
"Basilica di San Marco"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2015-03-05
. Iliwekwa mnamo
10 Februari
2016
{{
cite web
}}
More than one of
accessdate=
na
access-date=
specified (
help
CS1 maint: date auto-translated (
link
Marejeo
Italy - Eyewitness Travel Guides
. DK. 2005.
ISBN
1-4053-0781-1
Northern Italy - Insight Guides
. APA Publications. 2004.
ISBN
981-234-903-0
Hacken, Richard.
"History of Italy: Primary Documents"
. EuroDocs: Harold B. Lee Library: Brigham Young University
. Iliwekwa mnamo
6 Machi
2010
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
"FastiOnline: A database of archaeological excavations since the year 2000"
. International Association of Classical Archaeology (AIAC). 2004–2007
. Iliwekwa mnamo
6 Machi
2010
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
"Italy History – Italian History Index"
(kwa Italian na English). European University Institute, The World Wide Web Virtual Library. 1995–2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2021-08-15
. Iliwekwa mnamo
6 Machi
2010
{{
cite web
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
) CS1 maint: unrecognized language (
link
Viungo vya nje
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons
ina media kuhusu:
Italia
Online resources about Italy
Ilihifadhiwa
16 Desemba 2008 kwenye
Wayback Machine
at UCB Libraries GovPubs
Italia
katika Open Directory Project
Italian Higher Education for International Students
Ilihifadhiwa
19 Aprili 2009 kwenye
Wayback Machine
Italian National and Regional parks
Italian tourism official website
Ilihifadhiwa
18 Oktoba 2009 kwenye
Wayback Machine
Nchi za
Umoja wa Ulaya
Austria
Bulgaria
Eire
Estonia
Hispania
Hungaria
Italia
Kroatia
Kupro
Latvia
Lituanya
Luxemburg
Malta
Polandi
Slovakia
Slovenia
Romania
Ubelgiji
Ucheki
Udeni
Ufaransa
Ufini
Ugiriki
Uholanzi
Ujerumani
Ureno
Uswidi
Ulaya
Nchi huru
Albania
Andorra
Armenia
Austria
Azerbaijan
Belarusi
Bosnia na Herzegovina
Bulgaria
Udeni
Estonia
Georgia
Hispania
Hungaria
Isilandi
Eire
Italia
Kazakhstan
Kroatia
Kupro
Latvia
Liechtenstein
Lituanya
Luxemburg
Malta
Masedonia Kaskazini
Moldova
Monako
Montenegro
Norwei
Polandi
Romania
San Marino
Serbia
Slovakia
Slovenia
Ubelgiji
Ucheki
Ufalme wa Muungano
Ufaransa
Ufini
Ugiriki
Uholanzi
Ujerumani
Ukraine
Ureno
Urusi
Uswidi
Uswisi
Uturuki
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Abkhazia
Kosovo
Kupro ya Kaskazini
Ossetia ya Kusini
Transnistria
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
Akrotiri na Dhekelia
Åland
Azori
Faroe
Gibraltar
Guernsey
Jan Mayen
Jersey
Madeira
Man
Svalbard
nchi ya
Asia ya Magharibi
kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu ya
Ulaya
kiutamaduni
nchi ya kimabara
Rudishwa kutoka "
Jamii
Umoja wa Ulaya
Vigezo vya Ulaya
Nchi za Ulaya
Italia
Nchi za G7
Nchi za G8
Nchi za G20
Nchi za Umoja wa Ulaya
Mkataba wa Schengen
Umoja wa Forodha wa Ulaya
Maeneo ya Biblia
Nchi
Jamii zilizofichwa:
Kurasa zinazotumia marudio ya hoja katika wito wa kigezo
CS1 maint: date auto-translated
CS1 errors: redundant parameter
CS1 maint: unrecognized language
Italia
Weka mada
US